Apr 5, 2014

UCHAGUZI WA MWAKA 2015 KUTUMIA KATIBA MPYA


Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakipitia kabrasha la mapendekezo ya marekebisho ya baadhi ya vifungu vya kanuni za Bunge hilo mjini Dodoma jana. Kutoka kushoto ni Tundu Lissu, Ismail Jussa, Profesa Ibrahim Lipumba na Godbless Lema. 


Ikulu imeeleza kuwa imeshindwa kutimiza ahadi yake kwa taifa ya kulipatia Katiba Mpya ifikapo Aprili 26, 2014.
Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue alilieleza jana kuwa kwa hali ya mchakato huo ilivyo sasa, wameshindwa kufikia lengo hilo, lakini hawajakata tamaa kuhusu kupatikana Katiba Mpya ndani ya mwaka huu.
“Kweli matarajio ya awali yalikuwa hayo, lakini kama unavyoona hali ilivyo, ni vigumu kusema matarajio mengine, ingawa majadiliano yaliyofanywa mwaka huu ni lazima Katiba inayopendekezwa iwasilishwe kwa wananchi na mwakani tutakuwa na Katiba Mpya,” 
alieleza Balozi Sefue.
Katika hali isiyoeleweka Balozi Sefue alisisitiza msimamo wa awali wa Serikali kwamba Katiba itakayopatikana itatumika kwenye Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.

0 comments:

Post a Comment