Chad imetangaza kuwa itaondoa majeshi yake katika kikosi cha
kulinda amani cha Umoja wa Afrika huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, uamuzi
ambao utatoa pigo kubwa kwa juhudi za kurejesha amani katika nchi hiyo.
Jeshi la Chad lilikuwa mhimili wa kikosi cha kulinda amani cha Afrika katika nchi hiyo.
Wizara ya Mambo ya Nje wa Chad imetangaza kuwa Chad na Wachad wamekuwa wakilengwa katika kampeni chafu ya kuwatupia lawama za maafa yanayotokea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati licha ya kujitolea kwao.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa askari wa Chad watabakia katika maeneo yao katika nchi hiyo hadi pale mipango ya kuondoka itakapokamilika.
Hadi sasa pande nyingine zinazoshiriki katika operesheni ya kulinda amani huko Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yaani Umoja wa Afrika na serikali ya Ufaransa, hazijatoa tamko lolote kuhusu uamuzi huo wa Chad.
Wakati huo huo ofisi ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa idadi ya wakimbizi imeongezeka kutokana na kushadidi machafuko na mauaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu 60 wameuawa mjini Bangui katika siku kumi zilizopita.

0 comments:
Post a Comment