Apr 5, 2014

Sheikh Qasim: Mahakam za Bahrain hazifai

Ayatullah Sheikh Issa Qasim wa Bahrain, amesema kuwa, mahakama za nchi hiyo ni mbovu, kutokana na hukumu zilizotolewa hivi karibuni dhidi ya wanaharakati wa upinzani.
Sheikh Issa Qasim aliyasema hayo katika hotuba ya Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika msikiti wa Imam Swadiq (as) katika eneo la al-Deraz mjini Manama na kusisitiza kuwa, ni suala la kusikitisha kuona baadhi ya tawala za Kiarabu bado zinaamini kuwepo uadilifu nchini Bahrain. 

Amesema, katika hali ambayo baadhi ya tawala za Kiarabu zingali zinaamini hivyo, mahakama ya nchi hiyo imetoa hukumu kali dhidi ya wapinzani bila ya wao  kuwepo mahakamani na kupuuza kikamilifu sheria.

Kiongozi huyo wa kidini nchini Bahrain amehoji kwa kusema kuwa, ikiwa mahakama za Bahrain zina uadilifu, basi kwanini hukumu zote zimekuwa zikitolewa kwa maslahi ya utawala wa Aal-Khalifa dhidi ya wapinzani? 

Kwa upande mwingine Sheikh Issa Qasim amegusia suala la demokrasia nchini humo na kusema kuwa, utawala wa nchi hiyo huwa unajigamba kuwa eti unatekeleza demokrasia na kuongeza kama ninavyomnukuu: "Ni demokrasia gani hiyo inayokusudiwa?" mwisho wa kunukuu.

0 comments:

Post a Comment