Apr 4, 2014

Mkuu wa Mozila auzuliwa kwa kupinga liwati

Bodi ya kampuni inayotengeneza programu za Kompyuta ya Mozila ya nchini Marekani imemuuzulu Afisa Mkuu Mtendaji (C.E.O) kutokana na kupinga liwati na usagaji.

Brendan Eich amelazimika kuachia ngazi kutokana na mchango wake wa kifedha kwa makundi yanayopinga ndoa za watu wa jinsia moja. 

Mwaka 2008 Brendan Eich alitoa mchango wa dola 1000 kwa kundi lililokuwa likipinga kuidhinishwa uchafu huo katika jimbo la California nchini Marekani. 

 Ingawa afisa huyo mwandamizi wa Mozila amesema mtazamo huo wa kupinga liwati na usagaji ni wa kibinafsi, wakuu wa bodi ya shirika hilo wamesema ni vigumu kutofautisha mitazamo binafsi na rasmi kwa mtu wa kiwango cha CEO.

Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya majimbo ya Marekani yanayohalalisha ndoa za watu wa jinsia moja imeongezeka mno. 

Hadi sasa jumla ya majimbo 17 ya Marekani yameidhinisha ndoa za aina hiyo. 

Makundi ya kiraia ya kutetea ndoa za kawaida kati ya wanawake na wanaume huko Marekani zinasema viongozi wakuu wa nchi hiyo ndio wanaopaswa kulaumiwa kutokana na kuendelea kuhujumiwa taasisi za ndoa na familia.

0 comments:

Post a Comment