Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza wasiwasi
wake mkubwa juu ya hukumu ya kifo iliyotolewa ma mahakama ya Misri dhidi
ya mamia ya wafuasi wa Rais aliyepinduliwa na jeshi Muhammad Mursi.
Ban ameeleza wasiwasi wake huo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Nabil Fahmy mjini Brussels pambizoni mwa mkutano wa viongozi wa Afrika na Ulaya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia ametahadharisha kuhusiana na kukamatwa ovyo waandishi wa habari nchini Misri.
Mwezi uliopita mahakama ya Misri iliwahukumu adhabu ya kifo wafuasi 529 wa kundi la Ikhwanul Muslimin, hukumu ambayo imekosolewa sana na harakati za kutetea haki za binadamu nje na ndani ya Misri.

0 comments:
Post a Comment