ASKARI POLISI WA KITUO CHA MAGOMENI AKIUFUNUA MWILI WA MAREHEMU MTOTO FATUMA
Maiti ya mtoto aliyetambulika kwa jina la Fatuma Muhammed Bakar imeokotwa Asubuhi hii.
Maiti ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili imeokotwa leo hii pembezoni mwa mto wa Ng'ombe eneo la mwananyamala kisiwani jijini Dar es salaam.
Akiongea na munira blog,Diwani wa kata ya makumbusho Bwana Ally Haroub (Obama) ambaye anaishi jirani na alipookotwa maiti hiyo alisema,wapita njia wakiwa wanaenda katika shughuli zao walihisi kitu kutokana na harufu kali.
"Huu mwili wa marehemu umesombwa na mafuriko na hatimaye kuletwa hapa,ambapo wapita njia wameuona baada ya kusikia harufu kali"alisema
Munira blog ilishuhudia mwili wa mtoto huyo ukiwa umeharibika vibaya kutokana na kuoza.
Baba wa marehemu alikuwepo katika tukio hilo na kusema kwamba mtoto alikuwa anaishi Tandale yeye na mama yake wakati baba ni makazi wa mwananyamala kisiwani.
Polisi wa kituo cha Magomeni walifika na kuuchukua mwili wa marehemu fatuma kwa ajili ya kuupeleka Hospitali.
Hata hivyo gari hilo la polisi aina ya Land Rover lenye namba ya usajili T213AMV lilikwama kuondoka hatua chache baada ya kuupakia mwili wa marehemu kutokana na tope kali lililopo katika eneo hilo.
Hadi mwandishi wa habari hizi anaondoka gari hilo lilishindwa kutoka na kulazimika kuja gari jengine la polisi kwa msaada zaidi.
munira blog inawapa pole wazazi na ndugu wa marehemu fatuma.
BAADHI YA WANANCHI WAKIWA WAMEUZUNGUKA MWILI WA MAREHEMU.
0 comments:
Post a Comment