Apr 9, 2014

Polisi wa Misri wawashambulia wanachuo wa kike

Vikosi vya usalama vya Misri vimewashambulia wanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha al Azhar waliokuwa wakiandamana hapo jana katika uwanja wa chuo hicho kuilalamikia serikali ya mpito ya nchi hiyo. 

Katika maandamano hayo, wanachuo hao wa kike wametaka kurejeshwa madarakani Muhammad Morsi Rais halali wa Misri aliyeingia madarakani kwa njia ya kidemokrasia.
Misri imekuwa ikishuhudia maandamano ya wananchi wanaotaka kurejeshwa madarakani Morsi, huku takwimu za maafisa usalama wa nchi hiyo zikibainisha kuwa, watu wapatao 16,000 wamefungwa jela hadi sasa. 

Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limewakosoa maafisa wa Misri kwa kutumia mabavu dhidi ya raia wanaoandamana. 

Amnesty imesema watu 1400 wameuawa katika machafuko ya kisiasa tangu kupinduliwa Muhammad Morsi, vifo vingi vikiwa ni matokeo ya utumiaji mkubwa wa mabavu wa vikosi vya usalama dhidi ya raia.

0 comments:

Post a Comment