Apr 1, 2014

Hali ya machafuko yandelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Wanajeshi kutoka Ufaransa na wale wa kikosi cha Umoja wa Afrika Misca, wakipiga doria katika mji wa Bangui, nchini Afrika ya Kati.
Wanajeshi kutoka Ufaransa na wale wa kikosi cha Umoja wa Afrika Misca, wakipiga doria katika mji wa Bangui, nchini Afrika ya Kati.

Takriban watu 24 wameuawa na wengine yumkini 100 wamejeruhiwa na wanajeshi wa Chad katika mji mku wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, ambapo kwa sasa hali ya usalama imeendelea kuwa mbaya, licha ya juhudi zinazofanywa na kikosi cha kimataifa kwa kumesha mauaji.

Wanajeshi hao wa Chad wamewapiga risase juzi jumamosi raia wakati walipokua wakiwasafirisha ndugu zao kutoka Chad ambao wamekua wakiyakimbia machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

“Kuma miili 24 iliyookotwa na kuhesabiwa, na watu wengine ambao wamejeruhiwa vikali, katika mitaa ya kaskazini mwa mji wa Bangui”, meya wa wilaya ya Bégoua, Odette Dombolo, ameambia jana jumapili vyombo vya habari.

Mapema jana mchana , chanzo cha kikosi cha Umoja wa Frika Misca kilifahamisha kwamba watu wanane.

“Tunaendelea kuokota miili ya watu waliyouawa na idadi ya majeruhi inaendelea kuongezeka katika wilaya ya Bégoua na katika mitaa ya Gobongo na Galabadja, kwa sasa tuan kazi kubwa” ameendelea kusema Dombolo, huku akibaini kwamba kuna nyumba zilizochomwa moto baada ya kushambulia kwa roketi.

Dombolo amesema hasara ni kubwa kutokana na silaha zilizotumiwa.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na afisa wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika Misca, ambae hakutaka jina lake litajwe, “wanajeshi wa Chad walilengwa kwa grunedi ambayo imemjeruhi mmoja kati yao, na baadae wanajeshi hao walijihami.

Mmoja wa wasemaji wa kundi la wanamgambo wa kikristo la ant-balaka, brice Namsio, amekanusha tuhuma hizo, huku akibaini kwamba “ni uchokozi (...), hakuna alieshambulia wanajeshi wa Chad”.

0 comments:

Post a Comment