HILI NI MOJA YA JENGO LILILOBOMOLEWA KUAMKIA LEO
Askari wa jiji kwa kushirikiana na polisi wamebomoa baadhi ya majengo yaliyopo katika baadhi ya mitaa ya Kariakoo Jijini Dar es salaam.
Zoezi hili linaloenekana kuwa chungu kwa wamiliki wa majengo na wafanya biashara limefanyika usiku wa kuamkia leo.
Majengo yaliyobomolewa ni mapaa yaliyozidi mbele ya nyumba,fremu za biashara zilizo mbele ya nyumba na ngazi zilizo mbele ya nyumba.
Munira blog Asubuhi hii ilitembelea maeneo yaliyoathirika na kukuta mikokoteni na matoroli nayo yamekumbwa zoezi hilo.
Wakiongea kwa uchungu baadhi ya wafanya biashara wamesema zoezi hilo limewatia hasara kubwa,kwani baadhi ya maduka yao yamebomolewa na kuchukuliwa kila kitu.
"Hawa jamaa wamekuja na Tingatinga na kuanza kubomoa na kuvunja mabanda yetu ya biashara kama unavyoona ndugu mwandishi banda langu sijakuta bidhaa hata moja"alilalama mama mmoja bila kutaja jina.
Maeneo yaliyoathirika zaidi ni mtaa wa Kongo,Mchikichi na Agrey.
Wiki iliyopita mkurugunzi wa manispaa kupitia watendaji wake walipita mitaani na kutangaza kwamba manispaa ya ilala inawataka wafanya biashara wasitoe biashara zao ndani ya maduka yao.
WAFANYABIASHARA WAKIWA HAWAJUWI LA KUFANYA.
0 comments:
Post a Comment