Tanzania imeingia awamu ya pili
ya mpango wake wa mfumo wa matangazo kuhama kutoka analojia kwenda
dijitali, kwa kuzima mitambo ya analojia katika baadhi ya miji ya kati
na magharibi mwa nchi hiyo.
Mkuu wa mawasiliano wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania - TCRA, Inocent Mungy amesema mjini Singida kuwa kufikia Novemba 30 mwaka huu watakuwa wamezima mitambo ya analojia katika miji 11 kwa awamu hii ya pili, huku akidai kuwa kazi ya kukamilisha matangazo ya dijitali kwa nchi nzima itakuwa ndani ya muda uliowekwa.
Wakati Tanzania ikiwa mstari wa mbele katika eneo la Afrika Mashariki , Kenya ipo kwenye mgogoro wa kisheria kukamilisha mpango huo.
Kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa nchi nyingi duniani zinatakiwa kuhamia matangazo ya digitali ifikapo Juni mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment