Mar 31, 2014

24 wauawa kwenye mapigano mapya huko CAR

Watu wasiopungua 24 wameuawa na wengine 100 kujeruhiwa baada ya kuibuka mapigano mapya Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

 Odette Dombolo Meya wa Begoua amesema kuwa, wanajeshi wa Chad ambao waliingia nchini humo kwa shabaha ya kuwarejesha nyumbani raia wao walioko Jamhuri ya Afrika ya Kati waliwafyatulia risasi wananchi wa eneo la Begoua lililoko Bangui, mji mkuu wa nchi hiyo.
Mashuhuda wanasema kuwa, watu waliovaa sare za jeshi la Chad waliingia katika eneo hilo baada ya kuvuka mpaka wa nchi hizo mbili na kutekeleza shambulio hilo.

 Taarifa zinasema kuwa, mapigano yameongezeka nchini humo baada ya kuingia majeshi ya Chad ambayo ni sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati MISCA. 

Inafaa kuashiria hapa kuwa, tokea kushadidi mashambulio ya wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka dhidi ya Waislamu nchini humo mwezi Disemba mwaka 2013, maelfu ya watu wameuawa wengi wao wakiwa ni Waislamu na wengine zaidi ya laki saba kulazimika kuyakimbia makazi yao.

0 comments:

Post a Comment