Hatma ya sheria ya kunyonga inategemea maoni ya wananchi: Tanzania
Kusikiliza / Hamishia Wakati mkutano wa baraza la haki la Umoja wa mataifa ukiendelea mjini GenevaUswisi, Tanzaniaimesema ufutwaji wa hukumu ya kunyonga nchini humo kunategemea maoni ya wananchi na kwamba mchakato huo unaendelea licha ya shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa.Akizungumzia ripoti ya hali ya haki za binadamu iliyowasilishwa katika mkutano huo, mwakilishi wa kudumu waTanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva Balozi Modest Mero amesema nchi yake imekuwa ikizingatia demokrasia kwa kuwashirikisha wananchi kwa kila hatua ikiwamo masuala nyeti kamahilo.
Hata hivyo Balozi Mero amesema wizara ya Katiba na Sheria ndiyo inaratibu mchakato huo.
0 comments:
Post a Comment