Mar 25, 2014

AL SHABBAAB LKUENDELEZA MASHAMBULIZI

Kundi la al Shabab latishia kuongeza mashambulizi dhidi ya Amisom na mataifa jirani ya Somalia

Wanamgambo wa al Shabab wakiwa katika mazowezi, kando ya mji wa Mogadisco, novemba mwaka wa 2008.
Wanamgambo wa al Shabab wakiwa katika mazowezi, kando ya mji wa Mogadisco.

Wanamgambo wa kundi la kigaidi la al Shabab wametishia kwa mara nyingine kuendelea na mashambulizi dhidi ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom), hata katika ukanda wa Afrika ya mashariki na nchini Somalia, imetahadhari Umoja wa Mataifa.

Umoja wa mataifa UN umeonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa ongezeko la mashambulizi ya kushtukiza yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la Al-Shabab nchini Somalia wakati huu ambapo operesheni kubwa inafanywa kukabiliana na wapiganaji hao.

Balozi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Somalia, Nicholas Kay amesema kuwa licha ya operesheni kubwa inayoendelea kufanywa na vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM kuwadhibiti wapiganaji hao, bado wanamgambo wa Al-Shabab wameendelea kuwa na nguvu na kuzidisha mashambulizi yao mjini Mogadishu.

Kay amesema kuwa wanamgambo hao wameshajua kuwa wamezidiwa kwenye vita hivyo na ndio maana na wao wameendelea kuzidisha mashambulizi zaidi dhidi ya vikosi vya Serikali na wanajeshi wa AMISOM.

Kauli ya Kay anaitoa wakati huu ambapo vikosi vya AMISOM vimeendelea kufanikiwa kuchukua miji zaidi iliyokuwa inakaliwa na wapiganaji hao.

Mbali na nchini Somalia, Kay amesema wanamgambo wa Al Shabab wanatishia pia kuetekeleza mashambulizi katika nchi jirani na Somalia wakati huu wakiendelea kusambaratishwa.

Amisom ambao idadi yake imefikia wanajeshi 22.000, wameanza mashambulizi zaidi dhidi ya ngome na miji iliokuwa inakaliwa na Al Shabab tangu mwanzoni mwa mwezi March iliofaanikiwa kuiteka miji saba iliokuwa chini ya himaya ya wanamgambo wa Al Shabab.

0 comments:

Post a Comment