Mar 25, 2014

Wafuasi 529 wa Ikhwaan wahukumiwa kifo Misri

Mahakama moja mjini Cairo, Misri, imetoa adhabu ya kifo kwa wafuasi na wanachama 529 wa harakati ya Ikhwanul Muslimin walikokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji na kuvuruga amani.
Hukumu hiyo imelaaniwa na chama cha wanasheria nchini humo ambacho kimesema jeshi la Misri limerudisha udikteta ulioangushwa na wananchi mwaka 2011. 

Maandamano yamefanyika nje ya mahakama hiyo punde baada ya hukumu hiyo kutolewa.  

Mahakama imesema wafuasi hao wa Ikhwan wamehusika na mauaji dhidi ya maafisa wa usalama pamoja na kutatiza amani na utulivu ndani ya nchi. 

Wachambuzi wengi wanaitakidi kuwa hukumu hiyo ni ya kisiasa yenye lengo la kuwanyamazisha wakosoaji wa serikali. 

Serikali ya mpito ya Misri inayoungwa mkono na jeshi imeendeleza ukandamizaji dhidi ya wafuasi wa rais aliyepinduliwa, Mohammad Morsi, ukandamizaji ambao umeongezeka baada ya serikali kuliorodhesha kundi la Ikhwanul Muslimin miongoni mwa makundi ya kigaidi miezi kadhaa iliyopita.

0 comments:

Post a Comment