Mar 29, 2014

Serikali: Wananchi Libya wataka utawala wa Kiislamu

Waziri wa Vyombo vya Sheria nchini Libya ametangaza kuwa, Walibya wanataka kutekelezwa sheria za Kiislamu nchini mwao. 

Salah Al Marghani amesema kuwa, kutekelezwa sheria za Kiislamu nchini Libya ndilo chaguo la wananchi wa nchi hiyo.

Al Marghani ameyasema hayo katika kikao cha ufunguzi wa tume ya kuchunguza sheria nchini Libya na kuongeza kuwa, dini Tukufu ya Kiislamu imechunga kwa kiwango cha juu kabisa kila upande wa maisha ya mwanadamu.
 
Ameongeza kuwa, Wizara ya Vyombo vya Mahakama itaipatia tume hiyo ya kuchunguza sheria nchini humo kila suhula kwa ajili ya kufikiwa suala hilo. 

Shughuli ya tume hiyo ya kuchunguza sheria nchini humo ni kuainisha vipengee vinavyopingana na sheria za Kiislamu katika sheria za nchi hiyo na kuweka pahala pake sheria za Kiislamu.

Itakumbukwa kuwa, mwaka 1969 baada ya Kanali Muammar Gaddafi kufanya mapinduzi ya kijeshi na kushika madaraka, tarehe Pili Machi kwaka 1977 alitangaza kusimamishwa katiba ya mwaka 1951, na akaandika pahala pake kitabu kilichoitwa kwa jina la 'Kitabu cha Kijani' na kukifanya kuwa katiba ya nchi hiyo.

Wapinzani wa Gadafi wanasema kuwa kitabu hicho kiliotoa mwanya wa kuendeshwa siasa za kidikteta nchini Libya.

0 comments:

Post a Comment