Rais wa Marekani,Barack Obama,akiondoka katika mjini Rome, akijielekeza Saudia Arabia, machi 28 mwaka 2014
Barack Obama atakua nchini Saudia Arabia leo jioni. Ni zira
ya pili ya rais Obama nchini Saudia Arabia tangu alipochaguliwa
kuliongoza taifa la Amerika. Riyad ni mshirika kitambu wa Marekani,
lakini miezi hii ya nyuma, uhusiano kati ya mataifa hayo mawili
ulidorora, kutokana na kutoelewana kuhusu baadhi ya faili za kikanda,
vita nchini Syria, mapinduzi ya kijeshi nchini Misri,...
Watu sitini na tano muhimu waliyochaguliwa nchini Marekani
wamemuandikia Obama wakimuomba azungumze na mwenyeji wake, mfalme
Abdallah kuhusu masuala ya haki za binadamu, hali ya mwanamke katika
jamii ya raia wa Saudia.
Obama anafanya ziara nchini Saudia Arabia ili kujaribu kuboresha uhusiano uliyodorora miezi hii ya nyuma na taifa hilo.Utawala wa kifalme wa Saudia Arabia inailaumu Washington kukataa kuwapa silaha za nguvu waasi wa Syria, na kutounga mkono mapinduzi ya kijeshi nchini Misri.
Utawala wa kifalme wa Saudia Arabia imekua pia na wasiwasi na Marekani kuhusu mazungumzo na Iran.
Mazungumzo kati ya Israel na Palestine yamo katika agenda ya mazungumzo ya viongozi hao wawili.
Hayo yakijiri Riyad imekataa kumpa viza muandishi wa Jerusalem Post ili aweze kuhudhuria ziara hio, jambo ambalo Washington haikulifurahia.
Saudia Arabia ni ya pili kwa kuingiza kiwango kikubwa cha mafuta nchini Marekani, mataifa hayo mawili ya mekua na ushirikiano wa kutosha katika masuala ya usalama.
Obama anakabiliwa na kibarua kigumu cha kumuelewesha mwenyeji wake, mfalme Abdallah.
0 comments:
Post a Comment