Mar 27, 2014

Mazungumzo ya dini za mbinguni yaanza Qatar

Mkutano wa 11 wa kimataifa wa mazungumzo ya dini mbalimbali za mbinguni umeanza leo huko Doha mji mkuu wa Qatar ukihudhuriwa na  Maulamaa wa Kiislamu, Maaskofu  wa Kikristo  na Makuhani wa Kiyahudi. 

Mkutano huo unajadili na kuchunguza njia za kujenga umoja na mshikamano kati ya dini hizo za mbinguni, uhusiano wa vijana na dini na nafasi  za dini katika kuleta maendeleo duniani.

 Munir al Tlili Waziri wa Masuala ya Kidini wa Tunisia amesema kuwa, dini zinakabiliwa na changamoto nyingi na amewataka washiriki wa mkutano huo kuwazingatia zaidi vijana. 

Waziri Tlili amesema kuwa dini za mbinguni hazitofautiani bali zina mwelekeo wa kumwongoza na kumrekebisha mwanadamu kwa kutumia mbinu na njia  tofauti.

Naye Mark Cohen mhadhiri wa Uyahudi katika Chuo Kikuu cha Princeton nchini Marekani amesema kuwa, Mayahudi walikuwa wakiishi vizuri na kwa amani katika kipindi cha ustaarabu wa Kiislamu na kwamba kinyume na madai yanayotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel, kamwe Waislamu hawakuwahi  kuwakandamiza na kuwanyanyasa Mayahudi. 

0 comments:

Post a Comment