Mar 27, 2014

Magaidi washambulia kaburi la Swahaba Syria

Magaidi wanaowakufurisha Waislamu wengine wameendelea kushambulia maeneo matakatifu nchini Syria, ambapo wameharibu kwa mabomu makaburi ya swahaba wa Mtume Muhammad (saw) Ammar bin Yasir na mtukufu Uwais al Qarani katika mji wa Raqqa. 

Picha zilizorushwa katika mtandao wa intaneti zimeonesha eneo la msikiti lililokuwa na makaburi hayo, huku paa na kuta zake zikiwa zimeharibiwa kwa kiasi kikubwa na magaidi hao.

Shirika la Kusimamia Haki za Binadamu la Syria limesema kuwa, kundi la kigaidi linalojiita 'Utawala wa Kiislamu Iraq na Sham' (ISIL) lilishambulia eneo hilo tukufu la Waislamu kwa milipuko miwili mikubwa hapo jana.  

Makundi ya kitakfiri yenye itikadi za kufurutu ada, yameshambulia na kuharibu maeneo mengi ya kihistoria na Kiislamu nchini Syria kwa miaka mitatu iliyopita kutokana na itikadi zao potofu.

0 comments:

Post a Comment