Serikali ya Tanzania imesema
kuwa imebaini kuwepo kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto wa kike
kwenda nchini China kwa lengo la kuwashirikisha katika ukahaba ambao
unadaiwa kusababisha kunyanyaswa kwa wasichana hao na wengine kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimatifa nchini humo Bernard Membe amesema serikali itatuma wachunguzi nchini Uchina kuchunguza biashara hiyo.
Hatua hiyo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya msichana mmoja Mtanzania kuuawa kikatili katika mji wa Guangzhou nchini Uchina.
Waziri Membe amesema huenda baadhi ya wahusika wa bishara hiyo ni Watanzania wanaosafirisha wasichana wa dogo kwa kisingizio cha kuwatafutia ajira.
Baadhi ya wanaosafirishwa hujipata pabaya baada ya kuwasili Uchina ambapo hunyang'anywa hati zao za usafiri na kulazimishwa kushiriki ukahaba.
Baadhi ya wakaazi wa Dar es laam waliozungumza na BBC wameelezea kusikitishwa na vitendo hivyo na kuitaka serikali ichukue hatua.
0 comments:
Post a Comment