Kiranja wa wabunge wa chama tawala nchini Kenya amesema kuwa,
ngono za jinsia moja nchini humo ni tatizo sawa na ugaidi lakini akasema
kwamba, hakuna haja serikali kuchukua hatua zaidi dhidi ya suala hilo
kwani sheria zilizopo zinatosha.
Akimjibu mbunge Alois Lentoimaga aliyetaka kuchukuliwe hatua kali zaidi za kisheria dhidi ya liwati na usagaji kama ilivyofanya nchi ya Uganda, Aden Duale kutoka mrengo wa Jubilee amesema, Kenya inapaswa kupambana na suala hilo kama inavyopambana na ugaidi kwani ni tatizo kubwa kama yalivyo majanga mengine katika kijamii.
Duale amesema kuwa kesi 595 zinazohusu liwati na usagaji zimechunguzwa nchini Kenya tangu mwaka 2010 baada ya Katiba mpya kupasishwa, na mahakama zimewapata na hatia au kuwaachia huru watuhumiwa lakini polisi haijapata taasisi zinazotangaza mahusiano ya kujamiiana baina ya watu wenye jinsia moja kwa uwazi na kuvunja sheria.
Kiongozi wa wabunge wa chama tawala Kenya amesisitiza kuwa, hakuna haja ya kuchukua hatua kama zilizochukuliwa na Uganda kwani kuna Katiba na sheria ya jinai dhidi ya liwati na usagaji hivyo hakuna haja ya kuchukuliwa hatua kali zaidi.

0 comments:
Post a Comment