Magaidi 23 wa Daulatul-Islamiyyah fil-Iraq wa al-Sham-Daesh nchini Iraq, wameuawa na vikosi vya nchi hiyo katika operesheni mbili zilizotekelezwa na jeshi katika miji ya Kirkuk na Baqubah.
Duru za habari nchini Iraq zimetangaza kuwa, magaidi hao wameuawa baada ya kufanya shambulizi dhidi ya kambi moja ya jeshi katika maeneo ya al-Riyadh na al-Rashad magharibi mwa Kirkuk na kukabiliana na nguvu za jeshi hilo na kuuawa 10 kati yao.
Katika tukio jingine magaidi hao wa Daesh walivamia eneo la al-Suq katika viunga vya wilaya ya al-Sharqiyyah kusini mwa mji wa Baqubah.
Katika hujuma hiyo, jeshi la Iraq lilifanikiwa kuzuia hujuma na jinai za magaidi hao na kutokea mapigano makali yaliuyodumu usiku mzima wa kuamkia leo ambapo 13 kati yao wameuawa.
Jeshi la Iraq limesisitiza kuwa, litaendelea na operesheni zake kali dhidi ya magaidi wanaohatarisha usalama wa nchi hiyo ya Kiarabu.
Kwa mujibu wa viongozi wa Baghdad ni kuwa, baada ya magaidi kushindwa katika mapambano yao na jeshi la serikali halali ya Syria, sasa wameanza kuondoka nchini humo na kuelekea katika nchi kadhaa za jirani ikiwemo Iraq.
0 comments:
Post a Comment