Mar 24, 2014

Osman: Vyombo vya habari vinaipotosha jamii

Waziri wa Uwekezaji nchini Sudan, amekosoa mwenendo hasi wa vyombo vya habari vya kigeni kuhusiana na hali ya majimbo ya Darfur, magharibi mwa nchi hiyo. 

Mustafa Osman Ismail amesema, vyombo vya habari vya kigeni vimekuwa vikiakisi hali mbaya tu katika majimbo hayo kwa kuonyesha picha zisizostahiki, na kufikisha katika fikra za waliowengi ripoti zisizo na ukweli wowote.
Akiashiria athari mbaya na mwenendo na siasa za vyombo hivyo vya habari vya kigeni hasa katika miaka ya hivi karibuni, Ismail amesisitiza juu ya umuhimu wa kuungwa mkono wamiliki wa vyombo vya habari nchini Sudan, wakiwepo waandishi wa habari katika harakati za kudumisha usalama na amani katika eneo zima la Darfur nchini humo. 

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni serikali ya Khartoum ililifukuza shirika moja la kutoa misaada ya kibinaadamu la nchini
 Ufaransa lililokuwa likiendesha shughuli zake katika jimbo hilo la Darfur. Kwa mujibu wa taarifa ya serikali, shirika hilo lilikuwa likiendesha ujasusi na kudai eti linatoa misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa jimbo hilo.

0 comments:

Post a Comment