Mar 24, 2014

Waislamu waendelea kuuawa na Anti-Balaka CAR

Vikosi vya Kiafrika vilivyoko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati vimetangaza kuwa, kwa akali Waislamu wanne wameuawa na 

wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka mjini Bangui nchini humo. 
Askari mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake wa vikosi hivyo vya Kiafrika (MISCA) amesema kuwa, Waislamu hao wameuawa katika mapigano yaliyoibuka na wanamgambo hao na kwamba watu saba wengine wamejeruhiwa. 

Amesema kuwa mapigano hayo yamejiri katika maeneo tofauti mjini humo. 

Hayo yanajiri katika hali ambayo, hapo jana Askari hao wa kimataifa walioko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, walipambana vikali na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka. 

Mapigano hayo yaliwashirikisha askari wa kimataifa kutoka Burundi wanaojaribu kuzuia mashambulizi ya wanamgambo hao dhidi ya Waislamu.

 Alkhamis iliyopita kamanda mkuu wa vikosi vya Ufaransa nchini humo alitangaza kuwa, askari wa Ufaransa walipambana na Anti-Balaka katika njia ya Bangui kuelekea nchini Cameroon. 

Kwa upande mwingine askari hao wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, wametangaza kuwa, wanamgambo hao wa Kikristo wenye misimamo mikali, wanafanya njama za kushambulia msikiti mkuu wa Bangui.

0 comments:

Post a Comment