meli ya Korea Kaskazini “Morning Glory”, iliyokua ikibeba mafuta kinyume cha sheria.
Jeshi nchini Libya limefanikiwa kuwakamata wafanyakazi wote
wa meli ya Korea Kaskazini “Morning Glory” kufuatia usaidizi iliyoupata
toka kwa wanajeshi wa Marekani ambao walivamia meli hiyo.
Kukamatwa kwa
wafanyakazi hawa kunakuja ikiwa yamepita majuma kadhaa toka serikali ya
Libya itangaze na kuagiza vikosi vyake vya majini kushambulia meli hiyo
iwapo ingekataa kusimama na kurejea kwenye bandari ya Tripoli
inayosimamiwa na Serikali.
Meli hiyo ambayo imesheheni mafuta, ilifanikiwa kutoroka kwenye
bandari ya Al-Sidri na kuelekea kwenye bahari ya kimataifa hali
iliyosababisha kuondolewa madarakani kwa waziri mkuu Ali Zeidan kabla ya
wanajeshi wa Marekani kuingilia kati.Jeshi la majini nchini Libya, ambalo limekua likishikilia meli hio tangu jumamosi, limeikabidhi polisi ya uhalifu juzi jumapili wafanyakazi 21 wa meli hio, ambao ni kutoka mataifa mbalimbali, wakiwemo raia watatu wa Libya, ambao walikua ndani ya meli.
Kwa mujibu wa msemaji wa muendesha mashitaka mkuu wa Libya, al-Seddik al-Sour, nahodha ma meli na raia watatu kutoka Libya waliyokua ndani ya meli wamehojiwa jana.
Washington ilifahamisha jana kwamba ilikabidhi vyombo vya usalama vya Libya meli hio ambayo ilikua ikibeba mafuta yaliyonunuliwa kinyume cha sheria kwa waasi waliyojitenga wa mashariki mwa Libya.
Kulingana na taarifa ziliyotolewa na jeshi la majini la Libya, meli imewasili jana kwenye ufukwe wa bahari mjini Tripoli, kabla ya kujielekeza kwenye bandari ya Zawiya, kilomita 50 magharibi ya mji ili kupakua mzigo iliyokua inabeba.
0 comments:
Post a Comment