Mar 26, 2014

AU: Wanamgambo wa Anti-Balaka ni magaidi

Umoja wa Afrika (AU) umewatangaza wanamgambo wanaowashambulia Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwa ni magaidi na kueleza kuwa wanamgambo hao watahesabiwa kama wapiganaji adui, siku moja baada ya kumuua mwanajeshi wa kulinda amani wa Kongo.
Umoja wa Afrika umesema kuwa mwanajeshi huyo wa kulinda amani kutoka Jamhuri ya Kongo aliuawa katika mapigano ya juzi huko Boali umbali wa kilomita 80 kaskazini mwa Bangui. 

Wanajeshi wa AU baadae pia walifanikiwa kuwauwa wanamgambo 12 wa Anti-Balaka katika mapigano.

Hilo ni shambulizi la hivi karibuni kuwahi kufanywa na wanamgambo wa Anti-Balaka dhidi ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika (MISCA) huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

 Kikosi cha MISCA kimesema kuwa kinawachukulia wanamgambo wa Anti-Balaka kama magaidi na wapiganaji adui na kwamba wanapasa kushughulikiwa ipasavyo.

0 comments:

Post a Comment