Waziri Mkuu wa Tanzania
Mizengo Kayanza Pinda na baadhi ya mawaziri waandamizi wa serikali ya
nchi hiyo wamekumbwa na tuhuma za kuwahonga baadhi ya wajumbe wa bunge
maalumu la katiba kutoka kundi la watu 201 ili waunge mkono msimamo wa
serikali mbili.
Wenje aliwatuhumu pia, Mawaziri Profesa Jumanne Maghembe, Dakta
Shukuru Kawambwa na Gaudensia Kabaka kuwa wametoa rushwa za vyakula na
vinywaji kwa wajumbe hao.
Wakati huohuo, Makamu wa Pili wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Idd ametangaza vita kwa
mtu yeyote anayepanga njama za kuvuruga mchakato wa rasimu ya pili ya
katiba.
Balozi Seif Iddi aidha ameibeza kauli iliyotolewa juzi na Makamu
wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad kwenye viwanja vya
kibandamaiti na kusema kwamba kiongozi huyo hana uwezo wa kufanya
chochote visiwani Zanzibar.
Balozi Iddi ameonya kuwa, hali ikiendelea
hivyo Serikali ya Mapinduzi haitasita kuwashughulikia watu wote wa aina
hiyo.
0 comments:
Post a Comment