Feb 12, 2014

Amnesty: Waislamu wanafukuzwa nchini C.A.R

ukubwa wa hati 
Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limesema kuwa kuna operesheni za kufukuza jamii ya Waislamu kwa kuwaua katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, suala ambalo askari wa kulinda amani wa kimataifa wameshindwa kulizuia. 

Katika taarifa yake Amnesty imesema, shirika hilo lina kumbukumbu za kuuawa Waislamu wasiopungua 200 na wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka eneo la magharibi mwa nchi hiyo. 

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu aidha limesema, jamii nzima ya Waislamu imelazimika kukimbia na maelfu ya raia wafuasi wa dini hiyo ambao hawajaweza kukimbia wameuawa na kundi la Anti Balaka la Kikristo na kwamba Wakristo wanawachukulia Waislamu kuwa ni wageni na wanapaswa kuondoka nchini humo lengo ambalo linatimia.
 
 Hayo yamejiri huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akitahadharisha kuwa nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati iko kwenye hatari ya kugawanyika na kusema kuwa anapaswa kufanya jitihada za kuzuia ukatili, kuwalinda raia na kurejesha amani na utulivu nchini humo.

0 comments:

Post a Comment