Jan 21, 2014

Zoezi la kusambaza chakula CAR lakabiliwa na utata





Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilitangaza jana kuwa, halitaweza kusambaza chakula kikamilifu kwa wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na ukosefu wa amani katika maeneo mengi nchini humo.

Mkurugenzi wa Kanda wa WFP Denise Brown amesema kuwa, kuna malori kadhaa ya shirika hilo yanayobeba shehena za vyakula kwenye mpaka wa nchi hiyo na Cameroon ambayo bado hayajapata ruhusa ya kuingia Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na ukosefu wa usalama. Brown ameongeza kuwa zinafanyika juhudi za kupelekwa chakula hicho kwa wakimbizi kupitia njia  za anga.

Mkurugenzi wa Kanda wa WFP ameongeza kuwa, iwapo shehena hiyo ya vyakula itapelekwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa njia ya anga, kipaumbele cha kwanza kitatolewa kwa zaidi ya wakimbizi laki moja walioko kwenye kambi za wakimbizi karibu na uwanja wa ndege wa Bangui.

0 comments:

Post a Comment