Wanamgambo wa Boko Haram wa nchini Nigeria wamekishambulia kijiji
kimoja cha kaskazini mashariki mwa nchi hiyo katika jimbo la Borno na
kuwaua watu 18.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, mauaji hayo yamezusha wasi wasi mkubwa katika jimbo hilo. Vyombo vya usalama vya Nigeria vimethibitisha kutokea mauaji hayo.
Miongoni mwa wahanga wa shambulio hilo la Boko Haram katika jimbo la Borno ni wanawake na watoto wadogo. Mashambulio hayo yanatajwa kuwa ni wimbi jipya la vitendo vya machafuko lililoanza kushuhudiwa katika siku za hivi karibuni nchini humo.
Itakumbukwa kuwa, mwaka uliopita Rais Goodluck Jonathan alilifanyia mabadiliko jeshi la Nigeria, baada ya jeshi hilo kushindwa kukabiliana na wanamgambo wa Boko Haram ambao walikuwa wakifanya mauaji ya mara kwa mara dhidi ya raia wasio na hatia nchini humo.
Wakosoaji wa serikali ya Nigeria wanamlaumu Rais Jonathan wa nchi hiyo kwamba, ameshindwa kukabiliana na wanamgambo wa Boko Haram licha ya kutangaza hali ya hatari katika majimbo kadhaa likiwemo la Borno kwa lengo la kuendesha operesheni za kijeshi dhidi ya kundi hilo.

0 comments:
Post a Comment