Jan 21, 2014

Afghanistan yakosoa vikali siasa za Marekani

Msemaji wa Ofisi ya Rais wa Afghanistan amezikosoa vikali siasa za kindumakuwili za Marekani kuhusiana na vita dhidi ya ugaidi. 

Eimal Faizi ameelezea utata uliopo katika vita vya Marekani dhidi ya ugaidi na kuongeza kuwa, siasa na misimamo ya Washington katika kukabiliana na ugaidi ni za kinafiki, kwani licha ya kujua vyema zilipo kambi ya magaidi, haichukui hatua za maana za kukabiliana nao na wakati huo huo inashirikiana na nchi zinazounga mkono vitendo vya kigaidi.
Msemaji wa Ofisi ya Rais wa Afghanistan amesema kuwa, huwezi kulinganisha kundi la Taliban na vikosi vya kigeni vilivyoko nchini humo, kwani kundi la Taliban limeshasema wazi kuwa linafanya jinai na kutumia mabavu, lakini vikosi vya Marekani na vile vya Nato vinafanya unafiki, viliingia nchini humo kama nchi marafiki, 

lakini sasa vinatenda jinai za kuwauwa wananchi wasio na hatia kwa kujificha nyuma ya mgongo wa rafiki wa kiistratijia. 

Eimal Faizi amesisitiza kuwa vikosi vya kigeni badala ya kushambulia kambi za magaidi, vimekuwa vikishambulia makazi ya wananchi wasio na hatia wa Afghanistan.

0 comments:

Post a Comment