MKAZI wa Mburahati, Said Seif (39) amefariki dunia jijini Dar es Salaam baada ya kudondokewa na matofali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema kuwa
tukio hilo limetokea juzi saa 10:00 jioni eneo la Manzese wakati
mwanaume huyo alipobeba matofali mawili na kuyapeleka kwa mmiliki wa
mali hiyo, Rukia Said mkazi wa Manzese Sisi kwa Sisi.
Alisema kuwa Seif aliteleza kwa bahati mbaya na kuanguka chini na
matofali hayo yalimponda kichwani na kumsababishia maumivu makali na
kukimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala, ambako alifariki dunia
wakati akipatiwa matibabu.
Kamanda alisema kuwa maiti hiyo imehifadhiwa katika hospitali hiyo huku upelelezi wa tukio hilo ukiendelea.
Jan 8, 2014
Tofali Alilolibeba Lamuua
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







0 comments:
Post a Comment