Jan 8, 2014

Mtaalamu wa Maabara wa Chuo Kikuu DUCE Atekwa na Kuumizwa Vibaya

imageMATUKIO ya utekaji watu, kuwatesa na kuwatelekeza,yameanza tena baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, Bw. Joseph Yona, kutekwa, kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili na kutupwa eneo la Ununio, Tegeta, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kumakia jana baada ya watekaji hao, kumkuta Bw. Yona eneo Mtoni kwa Azizi Ally, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.

Bw. Yona alikuwa amekaa katika tawi la chama hicho na watu wengine sita wakiwa katika mazungumzo ya kawaida.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kitengo cha Taasisi ya Mifupa (MOI), kilichopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambako amelazwa, Bw. Yona alisema sababu ya kutekwa kwake na kutezwa ni baada ya kuitisha
mkutano na wahandishi wa habari.

"Mkutano huu niliuhitisha katika Hoteli ya Lamada, Ilala,Dar es Salaam uliokuwa ukijadili sakata la kuvuliwa uongozi Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe katika chama ndipo nilipoanza kutishwa kila wakati.

"Uongozi wa chama Makao Makuu ulitaka kuning'oa katika nafasi yangu lakini Kamati ya Utendaji ilikataa na kudai hawaoni kosa langu ni lipi...lilitoka agizo kwa viongozi wakuu wa chama kutaka ofisi yangu Temeke ifungwe," alisema.

Aliongeza kuwa, siku ya tukio saa 5 usiku akiwa eneo la Mtoni kwa Azizi Ally akizungumza na watu watatu, aliona kundi la watu sita likifika eneo hilo na kusema wanataka kumkamata yeye si watu wengine aliokuwa amekaa nao.

Bw. Yona alisema, alipowauliza wametumwa na nani kumkamata walidai ni maagizo ya viongozi wakuu wa CHADEMA, kutokana na mkakati wake wa kumuunga mkono Bw. Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho.

"Walinikamata na kudai wananipeleka Kituo cha Polisi Kati kwenda kutoa maelezo zaidi lakini nilishangaa kuona gari likipita kituoni na kwenda eneo ambalo sikulijua.

"Tulipofika eneo ambalo sikulifahamu, nilivuliwa fulana na kuzibwa machoni, walianza kunipiga na kunihoji wakinitaka niachane na shughuli za chama ili wasiniue," alisema.

Aliongeza kuwa, hakuweza kuwajibu kitu bali aliwaambia kuwa, kama wanataka maelezo zaidi kuhusu Kabwe waende wakamuulize mwenyewe kwani yeye hawezi kumsemea.

"Nilipojibu hivyo, mmoka kati ya watekaji alinipiga na kitu chenye ncha kali kichwani akiwa amenibinya sehemu zangu za siri...nilisikia maumivu makali nikawambia kwa nini mnaniua na mimi nina familia kama nyinyi.

"Muda huo tayari nilikuwa nimepigwa na kitu kizito, kupoteza fahamu hivyo walikimbia wakijua nimepoteza maisha, nilikuja kuamka saa 10 alfajiri na kujikuta niko peke yangu, nguo zangu zilikuwa zimetapakaa damu," alisema Bw. Yona.

Alisema baada ya kujitambua, alikwenda kugonga hodi katika nyumba ziliyopo jirani na eneo hilo ili kuomba msaada.

"Nilijitahidi kugonga milango milangu katika nyumba tatu lakini sikufunguliwa hivyo niliamua kujisogeza kidogokidogo ili nisubiri kukuche niombe msaada kwa watu wengine.

"Ilipofika saa 11 alfajiri, katia nyumba nilizogonga mlango kuna mtu alitoka, kunifuata na kuniuliza shida yangu ndipo nikamwambia...anilitaka nitaje namba ya mtu wangu wa karibu nikampa ya mdogo wake anaitwa Ayubu," alisema.
 

MOI wazungumza
Msemaji wa MOI, Bw. Patrick Mvungi, alisema walimpokea Bw. Yona saa 5 asubuhi akitokea MNH akiwa tayari amefanyiwa kipimo cha TC-SCAN hivyo bado anaendelea na matibabu.

Polisi watoa tamko
Kutokana na tukio la kutekwa Bw. Yona, ambaye ni kitaaluma ni Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Elimu (DUCE), Dar es Salaam, kupigwa na kujeruhiwa, Jeshi la Polisi Kanda

Maalumu limeanza kufanya uchunguzi wa kina.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema Bw. Yona alichukuliwa saa tano usiku katika Grosari ya Mgumbini,iliyopo wilayani Temeke, akiwa na wenzake watatu.

Alisema Bw. Yona na wenzake walikuwa wakinywa vinywaji ghafla walitokea watu sita waliojitambulisha kuwa wao ni Maofisa wa Polisi hivyo walimtaka waende naye Kituo cha Polisi cha Kati.

Hata hivyo, kati ya watu sita Bw. Yona aliweza kumtambua mmoja kwa sura na jina (jina limeifadhiwa), ambaye ni mwanachama mwenzake wa CHADEMA.

"Yona aliingizwa kwenye gari aina ya Land Cruiser, kumfungwa kitambaa usoni na kuondoka naye...watu hao walianza kumuhoji kwanini anaendelea kumshabikia Kabwe wakati ni mtu ambaye anakiharibu chama chao.

"Walitaka akawaoneshe rafiki yake ambae anajulikana kwa jina la Habibu Mchange, baada ya kuhoji kwanini apelekwi Polisi Kati, walianza kumshambulia na hatimaye kupoteza fahamu na kujikuta katika vichaka akiwa na majeraha usoni eneo la Ununio Tegeta, Dar es Salaam.

"Hatimaye usiku wa manane, Yona alipozinduka alijikuta yupo vichakani sehemu asiyoifahamu ndipo alipoanza kutangatanga na kutafuta msaada akiwa na maumivu makali katika mwili
wake," alisema Kamishna Kova.

Aliongeza kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha tukio hilo lina uhusiano wa moja kwa moja na mgogoro unaoendelea CHADEMA.

Alisema kabla ya tukio, Bw. Yona alikuwa katika hali ya hofu baada ya kupokea simu nyingi na ujumbe mfupi (sms) za vitisho kutoka kwa viongozi mbalimbali wa chama ambao wengine anawafahamu.

Kutokana na tukio hilo, jeshi hilo limeunda Jopo la Wapepelezi wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu, Jaffar Mohamed ili kuwabaini, kuwakamata watuhumiwa na kuwachukulia hatua za kisheria.


0 comments:

Post a Comment