Jan 8, 2014

Netanyahu: Waafrika lazima waondoke Israel


Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amedai kuwa, maandamano yanayofanywa na maelfu ya wahajiri wa Kiafrika wanaoishi Israel hayana faida yoyote.

Netanyahu amesisitiza kuwa, wahajiri na wakimbizi wa Kiafrika wanapaswa kuondoka Israel na maandamano na mikusanyiko inayofanyika haitakuwa na tija yoyote ile.


Wakati huo huo afisa mmoja wa Shirika la Umoja wa Mataifa lilaloshughulikia Wakimbizi UNHCR amesema kuwa, wahajiri wa Kiafrika waliotokea Eritrea na Sudan walioko Israel wanatambuliwa rasmi kuwa ni wakimbizi.

Siku ya Jumapili iliyopita, wahajiri wa Kiafrika walifanya maandamano makubwa mjini Tel Aviv wakipinga sheria mpya za kibaguzi zinazoviruhusu vyombo vya usalama vya Israel kuwafunga wahamiaji wa kigeni kwa kipindi cha mwaka mmoja bila ya kufikishwa mahakamani.

0 comments:

Post a Comment