Mkutano wa Kimataifa wa Mkutano wa Kimataifa wa Umoja
wa Kiislamu ulifanyika Tehran kuanzia tarehe 17 hadi 19 Januari kwa
mnasaba wa maadhimisho ya Maulidi ya Mtume Muhammad SAW na Imam Jaafar
Sadiq AS.
Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ilikuwa "Qur'ani na Nafasi
Yake katika Umoja wa Umma wa Kiislamu".
Mkutano huo ulioandaliwa na
Jumuiya ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu uliwaleta pamoja
wasomi, maualmaa na wanazuoni zaidi ya 300 kutoka nchi 50 za dunia.
Kutoka Kenya washiriki walikuwa ni Kadhi Mkuu wa zamani Sheikh Hammad
Qasim na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Kenya SUPKEM Profesa
Abdulghafur el Busaidi.
Mubarak Henia alipata fursa ya kuwahoji ili
kupata maoni yao kuhusu Umoja wa Kiislamu.
Bonyeza hapa chini kuyasikiliza mahojiano hayo..
0 comments:
Post a Comment