Jan 23, 2014

HABARI KAMILI YA WANAFUNZI 25 WALIOGONGWA MTWARA

 
 IMG-20140122-WA0004
 
Wanafunzi watano wa shule ya sekondari Mustafa Sabodo iliyopo nje kidogo ya mji wa Mtwara wamefariki Dunia na wengine 47 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari wakati  wakikimbia mchakamchaka mapema leo asubuhi.
 
Taarifa inasema kuwa gari hilo lenye namba za usajili T174 AED aina ya Mercides Benz lilikuwa likiendeshwa na Dereva Baraka Mgwegwe ambapo likiwa kwenye mwendo kasi liliacha njia na kuwagonga wanafunzi hao ambao walikuwa kandokando ya barabara wakikimbia mchakamchaka kurejea shuleni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Zelothe Steven na Mganga Mkuu wa hospital hiyo wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amewataja wanafunzi waliopoteza maisha kwa ajali hiyo ni pamoja na Khairati Mohamed Said.
 
Wengine ni Mwanahamisi Mohamed,Nasma Salum Mpunja, Hilda Matias Nguli na Farida Ally ambao wote wanasoma kidato cha kwanza katika shule hiyo.
 
Mpaka sasa hali za majeruhi 21  waliolazwa hospitalini hapo zinaendelea vizuri ukiondoa mmoja ambaye amehamishiwa katika hospitali ya mission Nyangao mkoani Lindi kwa matibabu Zaidi huku dereva aliyesababisha ajali hiyo akishikiliwa na polisi kusubiri sheria kufuata mkondo wake.
 
Dereva Baraka Mgwegwe amesema Nimetoka nyumbani kwangu sa 10 na nusu alfajiri naelekea kumpeleka Mgonjwa Lindi  Hospital nilikuwa na ndugu zangu wawili na mgonjwa kwenye gari.
 
tulipofika maeneo ya Pacha ya kwenda Mchuchu m.
 
Aliendeleza kueleza mbele yangu kulikua na lori imesimama na nyuma ya lori ndio kunasadikiwa kuwa kulikuwa na hao wanafunzi’
 
‘Mimi nilikuwa nimejiandaa kupishana na hiyo lori na wanafunzi nao wanaingia barabarani sehemu ambayo mimi nilikuwa najiandaa kupita mimi sikumuona mwanafunzi hata mmoja"
 
Alimaliza kwa kusema "kilichotokea pale nikutokea kwa hiyo ajali ya kuwagonga hao wanafunzi baada ya kuwagonga nikaenda kusimama kama mita 20 kutoka eneo la tukio nikatafuta usafiri wa piki piki nikaja kituoni hapa’.
 
  Baadhi ya wanafunzi waliolazwa hospital ya mkoa wa Mtwara kufuatia ajali hiyo.
IMG-20140122-WA0007
IMG-20140122-WA0009

0 comments:

Post a Comment