Jan 24, 2014

Makao makuu ya polisi Misri yalipuliwa kwa bomu


Habari kutoka Cairo, mji mkuu wa Misri zinasema kuwa, takriban watu 5 wameuawa na zaidi ya 45 wamejeruhiwa kufuatia mlipuko mkubwa wa bomu uliotokea kwenye jengo linalotumika kama makao makuu ya polisi nchini humo.
 
Habari zaidi zinasema gari lililokuwa na mada za milipuko lililipuka nje ya jengo hilo na kusababisha uharibifu mkubwa. Serikali ya Cairo inawatuhumu wafuasi wa Ikhwanul Muslimin kuwa ndio waliohusika na tukio hilo. 
Majuma kadhaa yaliyopitati serikali ya Cairo iliipiga marufuku harakati ya Ikhwani na kuiorodhesha miongoni mwa makundi ya kigaidi.

Mlipuko wa mjini Cairo umetokea siku moja kabla ya maadhimisho ya mwaka wa pili tangu kutokea mapinduzi ya wananchi ya Januari 25 mwaka 2011 yaliyomuondoa madarakani dikteta wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak. 

Usalama umeimarishwa na polisi imesema uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na shambulio hilo.

0 comments:

Post a Comment