Jan 5, 2014

BOTI YA KILIMANJARO II YAPATA AJALI NUNGWI,WATANO WAFA




 azam-2


Taarifa zilizopatikana ni kwamba boti ya Azam Marine, Mv Kilimanjaro imefanikiwa kuwasili Bandari ya Malindi licha ya kukumbwa na dhoruba kali eneo la Nungwi, dhoruba iliyopelekea baadhi ya mizigo kupunguzwa na mengine kuanguka baharini baada ya eneo la mbele ya Boti hiyo kuingiwa na maji kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka ya usafiri baharini.




 

Maiti wote wameletwa mjini kwa ajili ya kutambuliwa wapo katika hospitali ya Mnazi Mmoja. Serikali itaandaa utaratibu wa kawaida kwa maiti hizi kuzikwa ama kupewa jamaa zao.

Kepteni Nassor Abubakar Khamis ameshikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano.

Jumla ya abiria 396 walikuwemo katika manifesto ya safari hii kutoka Pemba kulekea Unguja.


Zoezi la kutafuta miili ya walioanguka baharini litaendelea kesho asubuhi baada ya kusitishwa kwa kuingia kiza.
Hivi karibuni mamlaka ya hali ya hewa iliwatahadharisha watumiaji wa bahari kuwa makini kutokana upepo mkali ukiotarajiwa kuvuma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Dk Khalid akizingumza na waandishi wa habari usiku huu. 
 


 

0 comments:

Post a Comment