Moja kati ya nyumba 14 katika Kijiji cha Shumba Mjini Wilaya ya
Micheweni ziliztoathirika kwa moto mkubwa ulitokea majira ya saa 5.00
asubuhi ya jumapili huku wakaazi wake wakichanganyikiwa kutokana na
maafa hayo.
Baadhi ya wananchi 100 ambao nyumba zao 14 zimeathirika na vibaya na
moto katika Kijiji cha Shumba Mjini wakipata hifadhi kwenye madrasa moja
Kijijini hapo.
Moja kati ya nyumba 14 zilizoathirika na moto katika kijiji cha Shumba Mjini ambapo wakaazi wake wakiwa wamechanganyikiwa kutokana na janga hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shehani Mohd Shehani akitoa tathmini ya awali ya uchunguzi wa moto uliotokea Shumba Mjini mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sei aliyefika kijijini hapo kuwapa pole wananchi walioathirika na maafa hayo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameiagiza Serikali ya
Mkoa wa Kaskazini Pemba kufanya tathmini mara moja nyumba zote
zilizoathirika kutokana na moto mkubwa uliokikumba Kijiji cha Shumba
Mjini leo majira ya saa 5.00 za asubuhi.
Nyumba zipatazo 14 zikiwa na wakaazi 100 zimeathirika vibaya kutokana na moto huo na nyengine 24
kuezuliwa mapaa yake kwa hofu ya kuathirika na moto huo ambao hadi sasa
kwa mujibu wa taarifa za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba
Shehani Mohd Shehani kwamba chanzo chake bado
hakijafahamika huku uchunguzi wa jeshi la polisi pamoja na vikosi
vyengine vya ulnzi ukiendelea.
Balozi Seif ambae pia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar akiwa kisiwani Pemba
kwa shughuli mbali mbali za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar alitoa agizo hilo muda mfupi baada ya kuwafariji wananchi wa Kijiji cha Shumba Mjini kutokana na maafa waliyoyapata ya janga la moto.
Akiwapa pole wananchi
hao 100 waliohifadhiwa kwenye madrasa mmoja Kijijini humo na baadaye
kupelekwa Skuli ya Kijiji hicho Balozi Seif aliwataka kuwa na subra
katika kipindi hichi cha mitihani na Serikali inajipanga kuangalia namna
ya kuwasaidia wananchi hao.
Alisema Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar itaandaa kikao maalum cha dharura keshokutwa
jumatatu ili kulijadili suala hili na kuona jinsi itakavyoweza kukusanya
nguvu za kuwasaidia wananchi walioathirika na janga hili.
0 comments:
Post a Comment