Hatimaye wanafunzi wa madrasa zinafofuata mtaala wa taasisi ya DYCC zilizopo katika mkoa wa Dar es salaam,jana walifanya mitihani ya muhula wa kwanza kwa mwaka 1435 Hijriyyah.
Munira blog ilishuhudia zoezi zima la mitihani hiyo iliyoanza saa tatu asubuhi na kumalizika saa kumi na moja jioni.
Jumla ya wanafunzi 1450 kutoka madrasa mbalimbali katika jiji la dar es salaam walishiriki mitihani hiyo huku wanafunzi hao wakionyesha furaha ya kwa kupata fursa hiyo.
Wakiongea na munira blog baadhi ya wanafunzi hao walionyesha matumaini yao juu ya mitihani hiyo.
namshukuru ALLAH kwani nimekikuta kile ambacho waalimu wangu walinfundisha kwa hiyo sina khofu zaidi ya kuwa namatuini mengi,kubwa tumuachie ALLAAH,alisema Maryam Muhammed Kutoka Munira Madrasa.
kwa upande wake ustaadh muhammad ambaye alikuwa ni msimamizi wa mitihani katika chumba namba mbili alisema "nawapongeza waandaaji kwani mitihani imeendana sawia na uwezo wa wanafunzi"
wakati huo huo ustaadh Abdul Muhsin kitumba wa madrasat Qaadiriyyah iliyopo mtaa wa shoka magomeni mapipa amesema "nawashauri viongozi wa idara wasiwe wanawarundika chumba kimoja watahiniwa wa madarasa mbalimbali"
Tumeshuhudia muda mwingi unapotea kwa wasimamizi wa mitihani kuchambua makabrasha kutokana na kuwakusanya watahiniwa chumba kimoja"
Kwa upande wake Sheikh Ramadha Kwangaya ambaye ni katibu mkuu Idara ya Madrasa DYCCC amesema tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa na kama yapo mapungufu basi ni ya kibin adam"
Jumla ya masomo kumi yalifanyiwa mitihani kwa darasa la kwanza hadi la tano.
BAADA YA MITIHANI WANAFUNZI WALIPATA FURSA YA KULA KAMA WANAVYONEKANA WANAFUNZI HAWA WA MUNIRA MADRASA
0 comments:
Post a Comment