Jan 21, 2014

'Nchi za Kiislamu zikabiliane na utumiaji mabavu'

Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezitaka nchi za Kiislamu zichukue hatua madhubuti za kukabiliana na utumiaji mabavu pamoja na misimamo ya kufurutu ada.

Ali Jannati ameashiria njama tofauti za maadui kwa umma wa Kiislamu na kubainisha kwamba, miongoni mwa njia za kukabiliana na njama hizo ni kufanyika mikutano kama huu uliomalizika siku chache zilizopita hapa mjini Tehran, wa Umoja wa Kiislamu

Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran ametoa wito wa kuweko juhudi maradufu katika ulimwengu wa Kiislamu za kukabiliana na njama za maadui dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Aidha Ali Jannati amesisitizia suala la kuweko juhudi za pamoja za kukabiliana na fikra za kufurutu ada.

0 comments:

Post a Comment