Jul 2, 2013

WANAFIKI NI KIKWAZO CHA MAENDELEO KWA WAISLAMU-SHEIKH KISHKI


  • ASEMA UNAFIKI NI UGONJWA HATARI KULIKO SARATANI,
  • ATAKA KILA MTU AJICHUNGUZE YUPO KATIKA KUNDI GANI.
Na mwandishi wetu wa munirablog.
Imeelezwa kwamba kusuasua kwa maendeleo ya waislamu nchini na duniani kote kunachangiwa kwa sehemu kubwa na wanafiki ambao wanatumiwa kuuhujumu uislamu kwa kutoa siri na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo ya waislamu.

Hayo yameelezwa na mhadhiri maarufu Sheikh Nurdin Muhammad Kishiki alipokuwa anawahutubia Waislamu waliofurika katika Msikiti wa Mtoro Jijini Dare s salaam usiku wa jana kuamkia leo.

Akiwasilisha mada ya Tofauti ya Waislamu na Wanafiki ikiwa ni muendelezo wa mihadhara ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Sheikh Kishki alisema,wanafiki ni tatizo kubwa sana katika uislamu wapo,walikuwepo na watakuwepo,hawa wanafiki ndiyo waliompa wakati mgumu sana Bwana Mtume S.A.W chini ya uongozi wa Abdillahi Bin Saluun.

Akifafanua maana ya unafiki alisema,Unafiki ni hali ya kuficha uhalisi wa jambo fulani na kudhihirisha kinyume na kilicho moyoni.

“Ndugu zangu Waislamu,dunia nzima kuna makundi matatu tu,makundi haya ni Waislamu,wasiokuwa Waislamu (makafiri) na Wanafiki,sasa ni wajibu wa kila muislamu anayemuamini na kumuogopa Mwenyezi Mungu na kuiogopa siku ya mwisho aiangalie nafsi yake ipo katika kundi gani miongonu mwa makundi hayo matatu”,mwisho wa kumnukuu.

Akitoa mifano kadhaa katika kubainisha ubaya wa wanafiki Sheikh Kishk alisema”,katika kuonyesha kwamba unafiki ni tatizo na Mwenyezi Mungu katutahadharisha sana juu ya hilo,katika Suratul Baqarah Aya mbili za mwanzo zimeeleza sifa za waumini na Mungu akasema kwamba hawa ndiyo walio ongoka na kufuzu,kisha katika aya ya tatu hadi ya tano Mungu akaelezea sifa za makafiri,lakini katika Aya kumi zilizofuata baada ya aya tano za mwanzo Mungu akaelezea kwa kina sifa na malengo yao wanafiki,sasa kwanini aya zote kumi ziwaelezee wao ilhali ni aya mbili tu zimewaeleezea waislamu,hii ni ishara wanafiki ni tatizo kubwa sana ndani ya waislamu”,alisema.

Huku akizisoma aya kadhaa kwa ustadi mkubwa ulioambatana na kuzichunga herufi sambamba na kuzipamba kwa mahadhi yenye kuvutia,Sheikh Kishki alisema,”Unafiki ni ugonjwa kwa mujibu wa Qur aan,tena ni gonjwa hatari sana kuliko ugonjwa wa ukimwi au saratani”mwisho wa kumnukuu.

Leo uislamu unasusua kwa sababu ya wanafiki wanatumika kuukwaza uislamu,lakini pamoja na hila zao nawatangazia wafahamu wazi kabisa kwamba hawatofanikiwa kwa mujibu wa ahadi ya mwenyeezi katika surat swafaa na surat tawbah,alisema.

Mihadhara ya kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan inaratibiwa na kamati ya maandalizi ya mihadhara ya Masjid Qiblataini chini ya Uenyekiti wa Sheikh Ally Bassaleh na leo kutakuwa na mhadhara katika msikiti wa Ibadhi mjini na mhadhiri atakuwa Sheikh Shaaban J.Mnyonge wakati kesho Inshaa Allaah kutakuwa na mhadhara katika msikiti wa Madina na Mhadhiri atakuwa Sheikh Walid Al had Omar.

Munirablog inawaomba radhi wasomaji wa blog hii kwa kuchelewa kuirusha taarifa hii,hii inatokana na tatizo la kimtandao.

SHEIKH KISHKI AKIHUDHURISHA MADA KATIKA MHADHARA WA KUUKARIBISHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN ULIOFANYIKA JANA KATIKA MSIKITI WA MTORO JIJINI DAR ES SALAAM.

BAADHI YA WAUMINI WALIOHUDHURIA MHADHARA HUO ULIOFANYIKA KATIKA MSIKITI WA MTORO JANA USIKU .

BAADHI YA VIONGOZI WA KAMATI YA MAANDALIZI YA MIHADHARA YA QIBLATAIN WAKIFUATILIA MADA IKIYOTOLEWA NA SHEIKH KISHKI.
KUSHOTO NI MWENYEKITI WA KAMATI HIYO SHEIKH ALLY BASSALEH NA KULIA NI SHEIKH AMIN AL HASSAN.



0 comments:

Post a Comment