Dec 14, 2013

SERIKALI YATAKIWA KUONDOSHA URASIMU BARAZA LA MITIHANI


 SHEIKH TWAHA SULEYMAN BANE (ANAYEANDIKA) MKUU WA KITENGO CHA DINI KATIKA AL HARAMAIN ISLAMIC CENTRE AKIWA NA MGENI RASMI DR KHALID WA MUNADHAMAT DAAWAT (ALIYEVAA SUTI) WAKIWA NA BAADHI YA VIONGOZI WENGINE KATIKA MAHAFALI YA WAKHITIMU WA KIDATO CHA SITA.



Serikali imetakuwa kuondosha urasimu uliopo katika Baraza la Mitihani la Taifa.

Hayo yapo ndani ya Risala iliyosomwa na wakhitimu wa Thanawy (kidato cha sita) kitengo cha dini wa shule ya Al Haramain Islamic Centre iliyopo Ilala Jijini Dar er salaam.


Akisoma risala hiyo hivi punde kwa niaba ya wakhitimu wenzake kijana Hassan Ramadhan Muhan amesema miongoni mwa changamoto walizo nazo wanafunzi wa kitengo cha dini ni pamoja na baadhi ya watendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kukataa au kuwa wazito kuvilinganisha vyeti vya wahitimu wanaotoka Al haramain Kitengo cha Dini.


 Hassan Ramadhan Muhan

Aidha alizitaja changamoto nyengine kuwa ni pamoja na kutokuwa na walimu wa kudumu.

"Kwa kipindi kirefu tumekuwa na walimu wa kujitolea tu na hii ina okana na kutokuwa na wafadhili wa kuwalipa walimu wetu,hii inaathiri ufanisi",alisema.

Jumla ya wanafunzi tisa wamekhitimu kiwango cha Thanawy (Kidato cha sita) kwa mwaka 2013.

Al haramain Islamic Centre kupitia kitengo cha dini,kimekuwa ni moja ya vituo vichache vya dini ya Kiislamu vyenye mafanikio makubwa licha ya kukabiliwa na ukata.

Kupitia kitengo hicho masheikh mabalimbali wamepatikana na kutapakaa ndani na nje ya nchi.

HAWA NI WAKHITIMU WA THANAWY MUDA MFUPI BAADA YA KUKABIDHIWA VYETI NA ZAWADI HIVI PUNDE.


SHEIKH KWANGAYA AKIOZUNGUMZA KWA NIABA YA WAZAZI.


0 comments:

Post a Comment