Dec 22, 2013

WAISLAMU WAHIMIZWA KUWA NA TABIA YA KUJISOMEA.


 Doctor Hamdun Ibrahim,akizungumza katika hafla ya kukabidhi vitabu kwa Taasisi zenye Maktaba.

Waislamu nchini wametakiwa kuzitumia vizuri fursa mbalimbali za kujipatia elimu.

Hayo yamesemwa leo hii na Mhadhir wa Chuo Kikuu Cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) DOKTA HAMDUN alipokuwa anatoa nasaha  katika hafla ya kukabidhi vitabu kwa maktaba za Kislamu.

Amesema "katika zama tulizo nazo fursa za kusoma ni nyingi mno ukilnganisha na zama zilizopita,hivyo ni vyema waislamu wakazitumia vizuri fursa hizo"
"Leo unaweza  kusoma hapo hapo ulipo kwa kutumia simu yako,au computer,au memori kadi n.k lakini pia unaweza kusoma kwa kwenda maktaba,hizi zote ni sehemu za fursa za kusoma".Alisema.

Pamoja na hivyo aliwaasa waislamu wasome kwa kuelewa na si kusoma kwa kuperuzi.

"Wataalamu wa elimu wanasema kuna kusoma aina nne,lakini aina bora ya kusoma ni kusoma kwa kuelewa kiasi kwamba hata usiku ukiwa unataka kulala akili inajirudia juu ya yale uliyo yasoma"mwisho wa kumnukuu.

Awali akizungumza katika hafla hiyo,mjumbe wa AN NAHL TRUST FUND Sheikh Yasin Kachehele alisema,lengo kuu la AN NAHL ni kuhamasisha maendeleo katika jamii hasa katika nyanja ya elimu na afya. 

Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa DYCCC Uliopo Living stone kariakoo,Dar es salaam.
 
 USTAADH MWINYI,AKISOMA QUR AAN TUKUFU.


BAADHI YA WASHIRIKI WA HAFLA HIYO WAKIFUATILIA JAMBO.


MWAKILISHI WA MAKTABA YA AL AZIZ ISLAMIC CENTRE YA MASASI AKIPOKEA VITABU KUTOKA KWA MGENI RASMI.





Ustaadh Muhammad ambaye ni mwakilishi wa idara ya madrasa DYCCC Akipokea vitabu kwa niaba ya idara ya madrasa.

0 comments:

Post a Comment