Dec 22, 2013

TAASISI YA AN NAHL YAMWAGA MSAADA WA VITABU.

MGENI RASMI DOKTA AMDUNI AKIMKABIDHI VITABU "FAT HUL BAAR"MWAKILISHI WA TAASISI YA ISLAMIC FOUNDATION

Taasisi ya AN NAHL TRUST FUND ya jijini Dar es salaam kwa kushirikiana na taasisi ya SPACE CHANNEL ya Saudi Arabia ,leo imetoa msaada wa vitabu mbalimbali vya dini ya kiislamu kwa taasisi zenye kuendesha maktaba.

ugawaji huo uliofanyika katika ukumbi wa DYCCC Uliopo kariakoo Jijini Dar es laam umemalizika hivi punde .


Akiongea katika hafla hiyo fupi mratibu wa zoezi hilo kutoka AN NAHAL Sheikh Said Bawazir amesema "An nahl kwa kushirikiana na taasisi ya SPACE CHANNEL ya Saudi Arabia tumeona tuziongezee nguvu maktaba chache zilizopo hapa chini ili waislamu wapate fursa ya kujisomea zaidi"mwisho wa kumnukuu

Jumla ya taasisi kumi na tatu na maimamu kumi na tano walifaidika na mgao huo.

Katika hafla hiyo fupi mgeni rasmi alikuwa Dokta Abdun Ibrahim akimwakilisha mkuu wa chuo kikuu cha kiislamu MUM Profesa Njozi.

MRATIBU WA HAFLA HIYO AMBAYE PIA NI MJUMBE WA AN NAHL TRUST FUND SHEIKH SAID BAWAZIR AKIONGEA JAMBO KATIKA HAFLA HIYO.




MGENI RASMI DOKTA SHEIKH AABDUN IBRAHIM AKIMKABIDHI SHEIKH SHIRARI BAADHI YA VITABU.













0 comments:

Post a Comment