Dec 23, 2013

Wivu Wasasbabisha Ulemavu




Hivi karibuni jijini mwanza mkazi mmoja wa Igoma Aliyefahamika kwa jina moja la Consolata amepigwa na mumewe na kung’atwa sikio na mtu anaedaiwa kuwa ni hawara wa mumewe.

Bi consolata amesema ulitokea ugomvi kati yake na mumewe ndipo hawara wa bwana alipokuja na kuingilia ugomvi huo kwa kumng'ata sikio na kuliondoa kabisa.

 
Mara baada ya kufanyiwa ukatili huo aliripoti katika kituo cha polisi lakini kwa madai yake ni kwamba watuhumiwa waliachiwa huru kwa sababu hasizo zijuwa,alisema.

kufuatia hali hiyo bi consolata alichukua hatua za kutafuta wasamalia wema ikiwemo waandishi ili waweze kumsaidia kupata haki.

0 comments:

Post a Comment