Hatua ya serikali ya Ufaransa ya kupeleka majeshi yake katika
nchi mbalimbali za Kiafrika, imewafanya Waislamu wachache katika nchi
hizo kuwa wahanga wa mashambulio ya majeshi ya nchi hiyo.
Mtaalamu wa masuala ya Ufaransa na Afrika ameiambia Kanali ya al Alam kwamba, uwepo wa majeshi ya Ufaransa barani humo umechangia kwa Wakristo wa Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kutenda jinai za kuwauwa Waislamu wachache katika mji huo.
Kwa upande mwengine, Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasihi wafuasi wao kukomesha vitendo vya chuki, kulipizana visasi na kumwaga damu za raia wasiokuwa na hatia.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Jumatatu ya tarehe 9 Disemba majeshi ya Ufaransa yalianzisha operesheni kamambe ya kuingia Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kisingizio cha kuwanyang'anya silaha wanamgambo wa makundi ya waasi nchini humo.

0 comments:
Post a Comment