Nov 28, 2013

MICHANGO YA MSIKITI WA KICHANGANI YAENDELEA



Michango ya msikiti wa Kichangani inaendelea vizuri na sasa imefikia shilingi milioni kumi laki tisa sabini na tisa elfu.(10,979,00/).

Hayo yalibainishwa Ijumaa iliyopita na Imamu wa msikiti wa Kichangani ambaye pia ni Mratibu wa michango hiyo Sheikh Omar Alhad.

Ndugu Waislamu,michango yetu imefikia Shilingi Milioni kumi na Laki Tisa Sabini na Tisa Elfu,tunawashukuru sana kwa michango yenu"alisema.

Aliendelea kusema "tunaomba tusichoke kuchangia bali tuongeze kasi zaidi kwani tufahamu ya kwamba sisi wenyewe ndiyo wanye wajibu wa kujiletea maendeleo"mwisho wa kumnukuu.

Michango hiyo ilianza mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka huu na ina lengo la kujiletea maendeleo ikiwemo kujenga Hospitali ya akina mama na mengineyo.

0 comments:

Post a Comment