
Rais wa Zambia, Michael Sata
Polisi nchini Zambia, wamemkamata na kumfungulia mashtaka
mwanasiasa wa upinzani Frank Bwalya kutokana na kumchafulia jina rais wa
Zambia, Michael Satta, baada ya kumfananisha na kiazi.
Kiongozi huyo wa
chama cha AllianceBwalya wakati mmoja alikuwa mfuasi wa rasi Satta.
Frank Bwalya, anakuwa mwanasiasa wa pili kujipata matatani baada ya mwansiasa mwingine wa upinzani , Nevers Sekwila Mumba wa chama cha Movement for Multiparty Democracy kuhojiwa na polisi mwaka uliopita kwa kumwita rais Satta mwongo.
Frank Bwalya anadaiwa kumtaja Rais Michael Sata kama "chumbu mushololwa", akimaanisha kiazi, kupitia kwa Redio siku ya Jumatatu.
Katika lugha ya Bemba, tamko hilo lina maanisha kiazi utamu ambavyo humegeka vinapopindwa , maana ya ndani ikiwa mtu ambaye hasikilizi ushauri wa wengine.
Hata hivyo, Bwalya ni kasisi wa zamani na mfuasi wa zamani wa Rais Sata, ingawa sasa anaongoza chama cha muungano wa vyama vya upinzani (Alliance for a Better Zambia (ABZ).
Naibu waziri wa mambo ya ndani, Stephen Kampyongo alisema kwamba, bwana Bwalya alikamatwa kwa kutoa matamshi ya kumharibia sifa Rais Sata.
Upinzani umetaka Bwalya aachiliwe ukisema kuwa yeye ni mwanasiasa asiyemuogopa mtu yeyote.
Wanasiasa wa upinzani, wamesema kua matamshi ya Bwalya,hayakua matusi.
Hali kwa sasa nchini Zambia ni ya mvutano kati ya upinzani na utawala.







0 comments:
Post a Comment