Nov 29, 2013

Mlipuko waua watu 40




Duru za habari nchini Libya zimeripoti kuwa, zaidi ya watu 40 wamekufa na wengine 15 kujeruhiwa katika mripuko wa ghala la kuhifadhia silaha linalomilikiwa na jeshi la nchi hiyo, katika mkoa wa Sabha. 

Mripuko huo umetokea wakati kundi la wakazi wa mji huo lilipokuwa linajaribu kupora zana za ghala hilo. 

Hadi hivi sasa hakujatolewa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo. 

Tukio hilo linajiri huku mapigano mapya yakiripotiwa kutokea kati ya jeshi la nchi hiyo na wanamgambo wa kundi la Answaru al-Sharia huko mjini Benghazi mashariki mwa Libya. 

 Mapigano hayo yameibuka baada ya wapiganaji wa kundi hilo kujaribu kuingia kinyemela mjini humo na kuzuiwa na jeshi. 

Serikali ya Tripoli hivi sasa inafanya juhudi za kuyashawishi makundi ya wabeba silaha kukabidhi silaha zao kwa

1 comments: