Oct 7, 2013

Waalim wa Madrasa ni Washauri Nasaha.


 USATAADH JAMAL MARINGO MTAALAMU WA ELIMU YA SAIKOLOJIA AKIWASILISHA MADA YA SAIKOLOJIA YA ELIMU.
Imeelezwa kwamba waalimu wa madrasa ni washauri Nasaha.

Hayo yamebainishwa hivi punde na mtaalamu wa Saikolojia Ustaadh Jamal Maringo alipokuwa anahudhurisha sehemu ya pili ya mada ya Saikolojia ya Elimu.

Amesema Seikolojia ya elimu ni pana sana na ina mfanya mwalimu awe ni mjuzi zaidi,kwa bahati mbaya waalimu wengi hawalifahamu hili.

"Wana semina naomba muelewe jambo muhimu sana,mwalimu wa madrasa asiishie kufundisha tu,mwalimu wa madrasa ni mshauri nasaha,sasa munawajibika kutoa ushauri nasaha katika maeneo yenu"alisema.

Aliendelea kusema kwamba,"leo ikitokea watu wa mtaa ambao wewe mwalimu upo au unaufanyia kazi wakawa nje ya utaratibu unaotakikana pasipo wewe kuwapa ushauri nasaha,fahamu kwamba utakuwa na Dhima mbele ya ALLAH".

Aliwataka waalimu kutanua utendaji wao na kuwashauri vijana wao kwa mujibu wa uwezo wao kitaaluma ikiwa ni njia moja wapo ya kuwasaidia.

Alisema jamii inayotuzunguka inakabiliwa na madhila mengi,ambapo mwalimu ana nafasi ya kutatua sehemu ya madhila hayo kwa kuwapatia ushauri nasaha wenye faida.

Aidha hakusita kueleza wakati yeye anasoma katika Madrasat Tanzania one ya Tandika walikuwa na utamaduni wa kushindana na madrasa mbalimbali katika fani ya dufu,lakini baada ya kupata ushauri nasaha vijana wengi miongoni mwao wakatumia muda huo kushindana au kujituma zaidi katika mambo ya kielimu,na sasa baadhi yao wana elimu kubwa sana. 

Semina hiyo ya siku tatu  iliyoandaliwa na World Islamic Call Society,inafikia kilele chake leo hii ambapo jumla ya washiriki 170 walihudhuria semina hiyo.

Kwa upande wake mratibu wa semina hiyo Sheikh Maulid Omar Kalyango amesema wana mshukuru ALLAAH kwa kuweza kulifikia lengo.

Aliongeza kwamba ni kawaida ya taasisi yao kufanya semina katika mikoa mbalimbali ila kwa mwaka huu hawatakuwa na semina nyengine kutokana na kuchelewa kupata fungu.

Naye Ustaadhi Ramadhan Abdallaah Pazi kutoka Al Haramain alisema,semina imemsaidia sana kwa kupata kujuwa asili faida,nafasi na matumizi ya lugha ya kiarabu hapa Duniani na kujuwa umuhimu wa elimu ya Saikolojia ya watoto,ambapo amesema ni ufumbuzi tosha wa changamoto za ufundishaji.

 BAADHI YA WANA SEMINA,MASHEIKH NA VIONGOZI WAANDAAJI WA SEMINA HIYO,WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA LEO HII KATIKA UKUMBI WA JAAFAR COMPEX ULIOPO UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM.

 SHEIKH MAULID OMAR KALYANGO AMBAYE NI MRATIBU WA SEMINA .

SHEIKH ABDALLAH BAWAZIR AKIJIBU MOJA YA MAWASWALI YA WANA SEMINA.

0 comments:

Post a Comment